Kuku wa kadai ( Kadai chicken)


Mahitaji
Nyama ya kuku isiyo na mifupa robo kilo
Pilipili hoho robo tatu kikombe
Kitunguu maji nusu kikombe cha chai
Nyanya zilizokatwakatwa kikombe kimoja cha chai
Mafuta ya kupikia kiasi
Pilipili iliyoiva moja
Bizari nyembamba iliyopondwa kijiko kimoja cha chai
Kitunguu saumu na tangawizi iliyopondwa kijiko kimoja
Chumvi kiasi
Unga wa garam masala uliochanganywa na unga wa pilipili na unga wa kadai kijiko kimoja cha mezani
Korosho punje kumi
Majani ya kotmir
Namna ya kupika
Chukua mafuta weka jikoni na kaanga vitunguu vyote pamoja na tangawizi. Kisha weka pilipili hoho endelea kukaanga na weka kuku. Weka viungo vyote vya unga na koroga vizuri vichanganyike.
Endelea kukaanga hadi aive. Baada ya hapo chukua nyanya zilizosagwa na kasha miminia kwenye mchanganyiko wako. Vikisha chemka, chukua korosho na saga zilainike kabisa kasha weka kwenye mchuzi wako. Weka kiasi cha maji yatakayotosha kuivisha na kisha weka pilipili. Acha vichemke kwa muda wa dakika kumi, mchuzi wako utakuwa tayari kwa kuliwa.
Ili kuoneza nakshi unaweza kupamba kwa majani ya kotmir na vitunguu maji


Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu