Posts

Kahawa ya baridi

Image
Mahitaji   Unga wa kahawa vijiko vine vya mezani   Unga wa kakao kijiko kimoja (kama utapendelea)   Maji ya moto vijiko vitano vya mezaniSukari vijiko vine vya mezani   Maziwa vikombe vitatu   Barafu kiasi Namna ya kutengeneza Chukua unga wa kahawa, changanya na unga wa kakao na kisha weka kwenye maji na chemsha hadi vichanganyike vizuri. Korogea sukari na acha iendelee kuchemka. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko wako wa kahawa na kisha changanya na maziwa na kisha saga kwenye mashine ya kusagia matunda. Mimina kahawa yako kwenye gilasi ndefu.   Juu yake weka ice cream unayopendelea. Lakini pia kuna namna ya pili ya kutengeneza ambayo utatakiwa kuchanganya viungo vyako vyote na kuvisaga kwenye mashine. Kisha utamimina kwenye gilasi na kuweka barafu juu yake. Hapo utakuwa umemaliza kutengeneza.

Wali wa kuaanga

Image
Mahitaji Kiporo cha wali wa Jasmine vikombe viwili vya chai Majani ya kitunguu maji   matatu hadi manne yaliyokatwa katwa Punje 3 -4 za kitunguu saumu kilichopondwa Sosi ya soya vijiko viwili vya chai Sosi ya samaki nusu kijiko cha chai Nyama ya samaki aina ya kaa Yai moja Sukari nusu kijiko Mafuta ya alizeti kiasi Vya kupambia Kipande kimoja cha ndimu Tango silesi mbili au tatu Sosi ya samaki, Pilipili ndefu na limao Namna ya kupika Chukua chuma cha kukaangia chapatti na weka mafuta kiasi na kisha weka vitunguu saumu na kanga hadi viwe vya hudhurungi. Kisha weka yai na endelea kukaanga hadi liive.   Weka nyama ya kaa na endelea kukaanga. Baada ya hapo miminia   wali na endelea kukaanga huku ukiuchanganya vizuri. Miminia sosi ya soya na halafu ya samaki kabla ya kunyunyizia sukari. Endelea kukaanga hadi viive vizuri kisha miminia majani ya vitunguu yaliyokatwa katwa. Hakikisha yanachanganyika vizuri na wali wako kabla ya kuumimina kwen...

Keki ya Pundamilia

Image
Mahitaji Sukari kikombe kimoja cha chai Mayai manne Maziwa kikombe kimoja cha chai Mafuta ya kupikia kikombe kimoja cha chai Unga wa ngano vikombe viwili vya chai Vanila matone matatu au unga wa hiliki nusu kijiko cha chai Unga wa kokoa nyeusi vijiko viwili vya chai Baking powder kijiko kimoja cha chai . Namna ya kuandaa Chukua sukari na weka kwenye bakuli lenye nafasi lenye uwezo wa kuchukua kiasi cha kilo moja na nusu hadi kilo mbili. Weka sukari na mayai na koroga hadi vichanganyike kabisa. Kama una mashine ya mkono ya kusagia unaweza kutumia. Weka maziwa na mafuta na endelea kuchanganya hadi vichanganyike vizuri Katika bakuli jIngine changanya baking powder, unga wa hiliki au vanilla pamoja na unga wa ngano. Weka huo unga kwenye mchanganyiko wako wa mayai na sukari kasha endelea kuchanganya. Gawa mchanganyiko sehemu mbili sawa Sehemu moja iweke pembeni na nyingine weka unga wa kakao na endelea kukoroga na uichanganye vizuri.. Mimina kwenye trey au s...

Kwa wale wa kupunguza uzito here we go!!!!!! Supu ya kabichi

Image

Upishi wa tembele la chukuchuku

Image
Mahitaji  Matembele mafungu 2 Nyanya 2 kubwa Kitunguu 1 Chumvi kiasi Mafuta kijiko 1 Ndimu 1 Namna ya kutengeneza Chukua matembele , yachambue na kisha yaoshe. Weka kwenye sufuria ya kupikia. Kata kata nyanya, kitunguu na weka juu yake. Kisha weka chumvi na mafuta na injika jikoni. Weka moto wa kiasi na acha viive kwa muda wa dakika tano. Funua na geuza, vitu vyote vitakuwa vimeiva. Kamulia ndimu na kisha ipua. Matembele yako yatakuwa tayari kwa kuliwa. Waweza kula na ugali ama chakula kingine utakachopendelea.

Afya yako ndio kipaombele chetu

Image
 Fanya mbogamboga na matunda kuwa sehemu ya maisha yako Tumerudi tena. Baada ya kutokuwepo hewani kwa muda , sasa tutakuwa tukikuletea mapishi mbalimbali kama ilivyokuwa awali. Tofauti na kipindi kile, tutakuwa pia tukikuletea dondoo mbalimbali za ulaji mzuri unaozingatia uboreshaji wa afya yako, pamoja na matukio mbalimbali yanayohusiana na mapishi pamoja na chakula kwa ujumla.

Wali wa dengu

Image
Mahitaji Mchele kilo moja Kitunguu maji kimoja kilichokatwakatwa Kitunguu saumu kimoja kilichosagwa Nyama robo kilo (kama unapendelea) Dengu robo kilo Chumvi kiasi Bizari kijiko 1 Unga wa mdalasini nusu kijiko cha chai Unga wa bizari nyembamba nusu kijiko cha chai Unga wa hiliki nusu kijiko cha chai Mafuta ya kupikia Namna ya kupika Anza kwa kuchemsha dengu zako hadi ziive kabisa. Na kisha chukua maji na injika jikoni yakichemka weka pembeni. Kwenye sufuria ya kwanza mimina mafuta ya kupikia na baada ya kupata moto weka vipande vya nyama na kanga taratibu. Weka viungo vyote ispokuwa bizari. Endelea kukaanga na vikisha chanyika vizuri miminia maji. Acha vichemke hadi viive kabisa. Baada ya maji kukauka ipua na kisha weka pembeni. Chukua sufuria nyingine na kisha weka mafuta ndani yake. Weka vitunguu saumu maji na halafu kanga hadi view vya hudhurungi. Weka mchele na endelea kukaanga. Miminia dengu zako katika mchanganyiko wako. Vikishachanganyika vizuri weka maji kia...