Posts

Upishi wa tembele la chukuchuku

Image
Mahitaji  Matembele mafungu 2 Nyanya 2 kubwa Kitunguu 1 Chumvi kiasi Mafuta kijiko 1 Ndimu 1 Namna ya kutengeneza Chukua matembele , yachambue na kisha yaoshe. Weka kwenye sufuria ya kupikia. Kata kata nyanya, kitunguu na weka juu yake. Kisha weka chumvi na mafuta na injika jikoni. Weka moto wa kiasi na acha viive kwa muda wa dakika tano. Funua na geuza, vitu vyote vitakuwa vimeiva. Kamulia ndimu na kisha ipua. Matembele yako yatakuwa tayari kwa kuliwa. Waweza kula na ugali ama chakula kingine utakachopendelea.

Afya yako ndio kipaombele chetu

Image
 Fanya mbogamboga na matunda kuwa sehemu ya maisha yako Tumerudi tena. Baada ya kutokuwepo hewani kwa muda , sasa tutakuwa tukikuletea mapishi mbalimbali kama ilivyokuwa awali. Tofauti na kipindi kile, tutakuwa pia tukikuletea dondoo mbalimbali za ulaji mzuri unaozingatia uboreshaji wa afya yako, pamoja na matukio mbalimbali yanayohusiana na mapishi pamoja na chakula kwa ujumla.

Wali wa dengu

Image
Mahitaji Mchele kilo moja Kitunguu maji kimoja kilichokatwakatwa Kitunguu saumu kimoja kilichosagwa Nyama robo kilo (kama unapendelea) Dengu robo kilo Chumvi kiasi Bizari kijiko 1 Unga wa mdalasini nusu kijiko cha chai Unga wa bizari nyembamba nusu kijiko cha chai Unga wa hiliki nusu kijiko cha chai Mafuta ya kupikia Namna ya kupika Anza kwa kuchemsha dengu zako hadi ziive kabisa. Na kisha chukua maji na injika jikoni yakichemka weka pembeni. Kwenye sufuria ya kwanza mimina mafuta ya kupikia na baada ya kupata moto weka vipande vya nyama na kanga taratibu. Weka viungo vyote ispokuwa bizari. Endelea kukaanga na vikisha chanyika vizuri miminia maji. Acha vichemke hadi viive kabisa. Baada ya maji kukauka ipua na kisha weka pembeni. Chukua sufuria nyingine na kisha weka mafuta ndani yake. Weka vitunguu saumu maji na halafu kanga hadi view vya hudhurungi. Weka mchele na endelea kukaanga. Miminia dengu zako katika mchanganyiko wako. Vikishachanganyika vizuri weka maji kia...

Vyakula 7 vitakavyokukinga dhidi ya athari za mwanga wa jua

Image
Kwa kawaida tumekuwa tukitumia cream na vipodozi kadhaa kukinga ngozi zetu dhidi ya athari zitokanazo na mwanga wa jua. Lakini je unafahamu kuwa kuna baadhi ya vyakula vinaweza kabisa kupambana na athari hizo bila msaada wa vipodozi. Kutokana na kutambua vizuri vyakula hivyo, nimeona si nikuletee ili upate kuelewa na ikibidi kutumia. Vyakula hivyo ni: Samaki wa maji baridi Matunda yenye rangi nyekundu na mboga za majani Mboga mboga za majani zenye rangi ya kijani iliyokolea Mafuta ya Lozi 'Olive Oil' Matunda yenye Vitamin C kwa wingi Chai ya kijani Choklet

Mkate wa mbogamboga

Image
Mahitaji Mbogamboga za kujazia Vitunguu vitatu vilivyokatwakatwa Nyanya 2 zilizokatwakatwa Hoho 1 ilikatwakatwa kitunguu saumu kilichopondwa kijiko 1 cha mezani Tangawizi iliyosagwa kijiko 1 cha mezani Unga wa bizari nzima kijiko 1 cha chai Sukari kijiko 1 cha chai Kotmiri fungu 1 Mafuta ya kupikia kiasi Chumvi kiasi Kwa mkate unga wa ngano vikombe 3 vya chai Hamiara kijiko 1 cha chakula Suakri kijiko 1 cha chakula Chumvi kijiko 1 cha chai Mafuta ya kula vijiko 2 Jibini kiasi Namna ya kuandaa Vya kujazia Chukua mafuta na weka kwenye sufuria kisha ijika jikoni. Anza kwa kuweka tangawizi na kitunguu saumu. Hakikisha unakaanga kuchelea kuungua. Weka kitunguu maji na endelea kukaanga. Sasa weka nyanya na kisha funika, ili kuruhusu nyanya hizo kuiva kwa mvuke taratibu. Katia hoho na baadaye unga wa binzari nzima, chumvi na pilipili kama utapendelea. Kwa mkate chukua kikombe cha chai. Weka maji nusu na kisha weka hamira chumvi na sukari. Acha viumuke vyenyewe kw...

Tambi za dengu

Image
Mahitaji Unga wa dengu ½ kilo Unga wa pilipili binzari nyembamba ½ kijiko cha mezani Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha chai Unga wa mchele ¼ kilo Chumvi kiasi Mafuta ya alizeti ½ lita Baking powder Namna ya kutengeneza Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa dengu. Kisha chukua nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi. Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga. Changaya vizuri na kisha weka maji kidogo kidogo huku ukukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye maandazi. Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika. Acha likae kwa muda wa nusu saa hadi saa moja. Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa. Kisha chukua mashine ya kupikia tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yaliyo jikoni. Weka kiasi kiasi huku ukikaanga. Acha mpaka zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri. Ipua na weka pembeni. Weka kwenye sahani safi na kavu. Tambi zako zitakuwa tayari ...

Sandwitch ya mchele

Image
Mahitaji Unga wa mchele 1/4kg Unga wa ngano 1/4kg Sukari 1/4kg Siagi 1/4kg Mayai 4 Maziwa 4 vijiko vikubwa. B.P 1 kijiko cha chai Namna ya kutengeneza Saga sukari na siagi. Tia mayai yaliyopigwa vizuri halafu tia maziwa. Nyunyiza unga wa ngano uliochungwa na mchele. Tia B.P katika vibati viwili vya sponge cake vilivyopakwa siagi Choma ukipenda paka jam baina ya katikati mbili.